JangaKenya
Kenya yasema rushwa ndio imechangia mlipuko wa gesi
2 Februari 2024Matangazo
Mlipuko huo ulisababisha vifo vya watu watatu usiku wa kuamkia leo na kuwajeruhi takribani watu wengine 300 mjini Nairobi.
Mlipuko huo umeteketeza ghala la nguo lililokuwa karibu na kuharibu magari kadhaa na mali za wafanyabiashara na makazi.
Akizungumza kutokea eneo la mkasa, msemaji wa serikali Isaac Mwaura amesema kituo hicho cha kujaza gesi kilikuwa kinyume cha sheria.
Mamlaka inayodhibiti nishati Kenya EPRA pia imesema ilikataa mara tatu maombi ya kampuni hiyo kupewa kibali cha kuweka kituo chake cha kuhifadhi na kujaza gesi katika eneo hilo ambapo mlipuko ulitokea kwa sababu, ni sehemu yenye wakaazi wengi.