1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kenya yawarudisha wakimbizi wa Uturuki makwao

22 Oktoba 2024

Umoja wa Mataifa umeelezea wasiwasi wake Jumanne kuhusu kurejeshwa makwao kwa wakimbizi 4 wa Kituruki kutoka Kenya ambao mashirika ya kutetea haki za binadamu yanasema walitekwa nyara na kurudishwa kwa nguvu.

https://p.dw.com/p/4m5af
Nembo ya Amnesty International
Nembo ya Amnesty InternationalPicha: Pond5 Images/IMAGO

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi,UNHCR, limesema hayo kwa shirika la habari la AFP kuwa limesikitishwa sana na hatua hiyo ya Kenya kuwatimua wakimbizi hao. Shirika lingine la Amnesty International nalo limeelezea tukio hilo kwamba linakiuka haki za binadamu na kuondoa uaminifu wa waomba hifadhi nchiniKenya. Hata hivyo, Wizara ya mambo ya nje ya Kenya ilisema imechukua hatua hiyo baada ya kupokea hakikisho kutoka Uturuki kwamba  wakimbizi hao watakuwa salama pindi watakaporejea.