Kenyatta, Ruto wafuatilia mashitaka yao ICC
5 Machi 2013Kenyatta na Ruto pamoja na mkuu wa zamani wa utumishi wa umma, Francis Muthaura, na mtangazaji wa redio, Joseph arap Sang, wanadaiwa kuhusika na ghasia za baada ya uchaguzi nchini Kenya miaka mitano iliyopita.
Tayari Muthaura na Arap Sang wameshakwenda mjini The Hague, lakini Kenyatta na Ruto wanatarajiwa kuhudhuria kikao hicho kwa njia ya mawasiliano ya vidio kutoka jijini Nairobi.
Ghasia hizo zilisababisha watu takriban 1,200 kuuwawa huku wengine zaidi ya 60,000 hadi leo wakiachwa bila makaazi. Kenyatta anapigania kuwa rais wa Kenya katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika tarehe 4 Machi, huku Ruto akiwa mgombea wake mwenza.
Kuhusu kile hasa kinachojadiliwa katika kikao hicho, mwenzangu Amina Abubakar amezungumza na Abubakar Yusuf ambaye ni wakili nchini Kenya.
Mwandishi: Amina Abubakar
Mhariri: Mohammed Khelef