1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KHARTOUM:Waasi wa LRA wakabiliwa na changamoto

8 Septemba 2005
https://p.dw.com/p/CEdJ

Makamu wa rais wa Sudan Salva Kiir akiwa nchini Uganda amependekeza kufanyike mazungumzo ya kituo ya kuwashawishi waasi wa Uganda wa LRA kuweka chini silaha.

Kiir ambaye pia ni rais wa serikali ya Sudan Kusini amesema iwapo mazungumzo hayo yatashindwa kufaulu waasi wa LRA watalazimika kuondoka kabisa kusini mwa Sudan ambako wanaishi.

Waasi wa LRA ambao wamekuwa wakiendeleza mashambulio dhidi ya rais wa Uganda wamewateka nyara maelfu ya watoto wa kiume na kuwaingiza jeshini na watoto wakike ambao wamewafanya watumwa wa bishara ya ngono.

Hata hivyo sasa waasi hao wanakabiliwa na changamoto kubwa kusini mwa Sudan kufuatia kumalizika kwa vita vya miongo miwili nchini humo mnamo Januari.