1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kifo chaitilia kiwingu furaha ya nahodha wa Uhispania

21 Agosti 2023

Nahodha wa timu ya taifa ya wanawake ya Uhispania na shujaa wao katika fainali ya Kombe la Dunia Jumapili Olga Carmona alifahamishwa kuhusiana na kifo cha babake mara baada ya mechi ya fainali ya jana dhidi ya England.

https://p.dw.com/p/4VPSN
Kandanda Kombe la Dunia 2023 Olga Carmona wa Uhispania
Olga Carmona akilibeba Kombe la Dunia la WanawakePicha: REUTERS

Haya ni kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Uhispania.

Carmona alifunga goli la pekee katika mechi hiyo kunako dakika 29ya mechi na kuwapa Uhispania taji lao la kwanza la Kombe la Dunia.

Na baada ya mechi hiyo, taarifa ya Shirikisho la Kandanda la Uhispania ilisema kuwa mchezaji huyo alifahamishwa kuhusiana na habari hiyo ya kuvunja moyo mara baada ya mechi.

Carmona mwenyewe alikuwa na haya ya kusema baada ya mpambano huo.

FIFA Kandanda la wanawake Kombe la dunia I Uhispania vs England
Olga Carmona akisherehekea goli lake katika fainali na EnglandPicha: Brendon Thorne/Getty Images

"Nafikiri tutatambua tulichokishinda mara tutakapotua nyumbani Uhispania ila naweza kusema kwamba tuna furaha sana. Tunashukuru kwa mapokezi mazuri muliyotupa na mazingira mazuri tuliyopata kutoka kwa wenyeji Australia na New Zealand. Tumefanya kitu cha kihistoria na kandanda la wanawake lipo hapa kusalia," alisema Carmona.

Kwa ushindi huo kila mchezaji wa Uhispania amepokea dola 270,000 huku shirikisho lao la kandanda likipata dola milioni 4.29.

Chanzo: DPAE/APE/Reuters