1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kijana wa miaka 20 ashitakiwa kwa ushoga Uganda

28 Agosti 2023

Kijana mmoja mwenye umri wa miaka 20 amekuwa raia wa kwanza wa Uganda kushitakiwa kwa vitendo vilivyokithiri vya mapenzi ya jinsia moja, kosa lenye adhabu yake kifo kwa sheria dhidi ya mapenzi ya jinsia moja nchini humo.

https://p.dw.com/p/4VfLx
Yoweri Musevini to sign anti-LGBT law
Picha: Themba Hadebe/AP/picture alliance

Kulingana na hati ya mashitaka iliyoonekana na shirika la habari la Reuters, kijana huyo alishitakiwa Agosti 18 kwa kosa la kushiriki mapenzi ya jinsia moja na mwanamme mwenzake mwenye umri wa miaka 41.

Hata hivyo, hati hiyo haikufafanua ni kwa nini kitendo hicho kilichukuliwa kuwa ni kibaya.

Soma zaidi:Benki ya Dunia yakemea sheria ya Uganda dhidi ya mashoga
 UN: Uganda lazima ifute sheria yake mpya ya kupinga ushoga

Kwa kuwa kosa lenye adhabu ya kifo husikilizwa Mahakama Kuu pekee, mshitakiwa huyo alisomewa mashitaka na kurudishwa rumande, kwa mujibu wa msemaji wa Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka, Jacqueline Okui, aliyezungumza na Reuters. 

Wakili wa mshukiwa huyo, Justine Balya, alisema anaamini kwamba sheria hiyo nzima inakwenda kinyume na katiba.