1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kina cha maji katika Ziwa Turkana kimeongezeka

7 Novemba 2024

Katika miaka ya hivi karibuni, kina cha maji ya Ziwa Turkana kimeongezeka na kuyatatiza maisha ya wanakijiji na wavuvi. Baadhi wamelazimika kusogea na idadi ya samaki imepungua kwani wanajificha kwenye maji ya mbali.

https://p.dw.com/p/4mkSO
Ziwa Turkana
Ziwa TurkanaPicha: Thelma Mwadzaya/DW

Ziwa hilo la Bonde la Ufa ndilo kubwa zaidi la maji ya chumvi duniani. Kenya na Ethiopia zina mpaka wa pamoja wa Ziwa Turkana na mito ya bonde la Omo inamimina maji yake humo. 

Mji wa Kalokol ni sehemu ya wavuvi kupakua samaki wao

Kina cha maji ya Ziwa Turkana kinaendelea kuongezeka na vijumba vimejikuta vikifunikwa na maji japo viko ufukweni. Wakaazi wamelazimika kuhama kwani wanahofu kwamba huenda Kalokol itasombwa na maji.

Uvuvi nao umetatizika kama anavyoelezea Philip Kamais, mfanyabiashara wa samaki,Samaki wamepungua kidogo lakini kwa sasa hali inaanza kubadilika.Hii ni kwasababu ziwa linashusha maji kwani kina kimeongezeka.Likitulia,mambo yatajipa.Hili limewahi kushuhudiwa awali katika mwaka wa 76 na 77 .Mwaka huu nao maji yamekuwa yakijaa na kukupwa lakini kina kimeongezeka,” anasimulia.

Ziwa Turkana li hatarani - UNESCO

Fukwe za Eliye zimejaa maji 

Katika eneo la Eliye, sehemu ya ufukweni imejaa maji. Hakuna tena sehemu ya kubarizi. Ziwa Turkana ni la pekee kwenye eneo la jangwani barani Afrika.

Johari ya kaskazini kama linavyoitwa lina urefu wa kilomita 250 kutokea mpaka wake na Ethiopia hadi kaunti ya Turkana. Ujenzi wa bwawa la Gibe katika nchi jirani ya Ethiopia ulitiliwa shaka kuwa harakati hizo zitaathiri maisha ya jamii za wafugaji, wakulima na wavuvi wanaoishi pembezoni mwa Ziwa Turkana na kuchangia migogoro kwasababu ya kusaka sehemu za malisho, kuathiri uvuvi kwani idadi ya samaki itapungua na kilimo kwavile kiwango cha chumvi kitaongezeka na kina cha maji kitapungua.

Soma: Ziwa Turkana liko hatarini-UNESCO

Christine Arot in mkaazi wa Todonyang iliyo karibu na ufuoni mwa Ziwa Turkana, lakipi pia ni mchuuzi wa samaki na ,”Wanaume wanavua na sisi wanawake tunawaandaa samaki hapo kando na kuuza.Hapo tuliko Todonyang’ ni mpaka wa Kenya na Ethiopia.Wakati kuna vita vinavyosababishwa na sehemu za kutekea maji na malisho biashara inatatizika.Kukiwa na amani, biashara inaendelea vizuri tukiwa na watu wa Ethiopia ambao ni majirani,” anafafanua.

Ifahamike kuwa jina la mji wa Kalokol lina asili yake kwenye lugha ya Turkana lililo na maana ya sehemu ya samaki wengi.Baada ya Kenya kujinyakulia uhuru wake kutoka kwa mkoloni, baba wa taifa Jomo Kenyatta alilipa ziwa hilo lililoitwa Rudolf jina la Turkana kwasababu ya wakaazi wa hapo.Hata hivyo waTurkana huliita ziwa hilo Anam Ka'alakol na maana yake ni bahari ya samaki wengi.

Mabadiliko ya tabianchi yaathiri misimu ya mvua

Ijapokuwa Mvua hazikunyesha kwa misimu minne mfululizo, kina cha maji ya Ziwa Turkana na mengine ya bonde la ufa kinaongezeka.

Mabadiliko haya yalianza kushuhudiwa miaka mitatu iliyopita. Ripoti ya serikali ya Kenya ya mwaka 2021 imekisia kuwa eneo la Ziwa Turkana limeongezeka kwa asilimi 10 kati ya mwaka 2010 na 2020.

Kamais Kennedy ni mfanyabiashara wa samaki mjini Kalokol na ana wasiwasi maji ya ziwa yatawatatiza zaidi kwavile,”Maji yamekuja kwa wingi.Hivi yamesogea umbali wa kama kilomita 2 na kijiji kilichokuwa hapa sasa hakipo tena na wanakijiji kiasi ya alfu 5 wameyakimbia makaazi yao.Kibiashara tumeathirika maana samaki wamepotea ,sio vile ilivyokuwa,kwani maji yakiongezeka samaki wanasogea mbali zaidi.Pili, mamba nao wameongezeka na wanajikuta kwenye sehemu ambazo binadamu wanaishi,” anaeleza.Wafugaji wageukia kilimo nchini Kenya

Mamba wa mto Nile walioko Turkana ni hatari zaidi

Kulingana na utafiti, idadi kubwa ya mamba wa mto Nile inapatikana kwenye ziwa Turkana.Mamba wa mto Nile ni moja ya aina ambazo ni hatari zaidi duniani wanaosababisha maafa ya binadamu.Mamba wa aina hii wana uwezo wa kuishi kwenye mito na maziwa ya maji ya baridi au ya chumvi.

Kuongezeka kina cha maji ziwa Turkana

Mikoma kuzama majini ni tukio la kawaida kwenye fukwe za ziwa Turkana tangu kina cha maji kiongezeke.Ripoti ya hivi Karibuni ya shirika la Umoja wa mataifa la mazingira, UNEP, inatahadharisha kuwa mabadiliko ya tabia nchi huenda yakakiongeza zaidi kina cha maji ya Ziwa Turkana.