Kiongozi wa upinzani nchini Senegal Ousmane Sonko ashtakiwa
1 Agosti 2023Watu wawili waliuawa katika maandamano hayo. Sonko, mgombea urais na mkosoaji mkali wa Rais Macky Sall, amekabiliwa na msururu wa matatizo ya kisheria, ambayo anadai kuwa yamekusudia kumfungia nje ya siasa za nchi.
Alikamatwa Ijumaa kwa tuhuma mpya zinazohusishwa na kauli alizotoa, mikutano ya hadhara aliyofanya, na matukio mengine tangu mwaka wa 2021.
Mashtaka mapya yanajumuisha kuhujumu usalama wa taifa
Mashitaka mapya yanajumuisha kuhujumu usalama wa taifa, ushirika wa uhalifu na kundi la kigaidi, kusambaza habari za uwongo na wizi. Mara baada ya kushitakiwa, waziri wa mambo ya ndani akatangaza kuwa chama chake cha PASTEF kitavunjwa kwa kuitisha uasi mara kwa mara, hatua iliyosababisha uharibifu na vifo. Chama hicho kimelaani hatua hiyo, kikisema kuwa uthabiti wa nchi hiyo sasa umeathirika