1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Alexei Navalny ahukumiwa miaka mingine 19 jela

5 Agosti 2023

Kiongozi wa upinzani na mkosoaji mkubwa wa serikali ya Urusi Alexei Navalny amehukumiwa miaka mingine 19 jela kwa makosa yanayohusiana na itikadi kali.

https://p.dw.com/p/4Uo0P
Alexei Navalny
Alexei NavalnyPicha: Evgeny Feldman/AP Images/picture alliance

Hukumu hiyo dhidi ya Navalny, ambaye aliitisha maandamano makubwa dhidi ya Rais Vladimir Putin, inatolewa katikati mwa ukandamizaji dhidi ya wapinzani.

Katika taarifa aliyoitoa kupitia Ukurasa wa Facebook, Navalny amewahimiza Warusi kuendeleza mapambano. Kesi hiyo ilikuwa ikisikilizwa kwa faragha katika gereza lenye ulinzi mkali liliko mashariki mwa mji wa Moscow.

Soma zaidi: Navalny amkejeli Putin, ''Mfalme yuko uchi''

Kiongozi hyuo wa upinzani tayari anatumikia kifungo cha miaka 9 jela kwa makosa ya ubadhirifu, mashitaka ambayo wafuasi wake wanadai kwamba yalichochewa na hatua ya Navalny kumpinga Putin.

Marekani na Ujerumani zimelaani hukumu hiyo zikisema ni ukosefu wa haki huku Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa na Uingereza zikishinikiza mwanasiasa huyo kuachiwa.