Kivuli cha ukoloni wa Ujerumani - Sehemu ya Kwanza
Historia
Shisia Wasilwa
19 Machi 2024
Kufikia mwaka 1885, mfanyibiashara wa Ujerumani alifanikiwa kununua pwani nzima ya Kiafrika. Alifanya hivyo kwa kutumia bunduki chache alizokuwa nazo pamoja na mkataba wenye hila. Mkataba huo pamoja na mikataba mingine barani Afrika ilifuangua mwanya kwa utawala wa kikoloni wa Ujerumani.