1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kolombo:Waasi wafunga maji baada ya kushambuliwa kwa ndege.

28 Julai 2006
https://p.dw.com/p/CG3B

Huko nchini Sri Lanka kiasi cha waasi sita wameuwawa na watu wanane wamejeruhiwa, wakati ndege za kivita za Sri Lanka zilipoishambulia kambi ya wapiganaji wa Tamil Tiger.

Vyanzo vya habari vya kiafisa vimekubali kuwa kulizuka mapigano mapya katika jimbo la Trincomalee lakini chanzo hicho hakikutaja maafa yoyote.

Ndege hizo za kivita zimeshambulia baada ya kuwa na uvumi kuwa jeshi la Sri Lanka litafanya shambulio la kushtukiza kwa kundi hilo la Tamil Tiger, wanaolidhibiti eneo kubwa la kaskazini na mashariki mwa mji nchini Sri Lanka.

Wakati huo huo kumeripotiwa kutokea mapigano ya risasi kati ya waasi wa Tamil na serikali huko mashariki mwa kisiwa hicho kunako sehemu ya usambazaji maji.

Serikali inawalaumu waasi kwa kuyafunga maji nakupelekea maelfu ya wakulima kukosa huduma hiyo katika maeneo yanayodhibitiwa na serikali, kwenye kitongoji cha Trincomalee.

Waangalizi wamesema zaidi ya watu 800 wameuliwa mwaka huu katika mgogoro wa waasi wa Tamil.