Kombora la India Agni V lafanikiwa
19 Aprili 2012Kombora lililopewa jina la Agni-V, likimaanisha moto linaweza kusafiri umbali wa kilometa 5000 sawa na maili 3100, likiwa linahitaji betri ya majaribio kabla ya kukamilisha hatua kadhaa na kuhifadhiwa katika ghala ya silaha.
Majaribio hayo yanaliweka taifa hili katika mataifa yenye nguvu na yaliyosonga mbele kisanyansi ulimwenguni. Waziri wa Ulinzi wa India A.K. Antony amesema kwa kufanikisha jaribio hilo, sasa taifa lao limekuwa ni miongoni mwa mataifa yenye nguvu.
Mafanikio hayo ya India yamekuja siku chache baada ya Korea Kaskazini kufanya jaribio lake lililokosa mafanikio kwa kuruka umbali usiozidi kilometa 100.
Ulimwengu umestajabishwa na tukio hilo kwani kwa sehemu kubwa ni Korea ya Kaskazini iliyodhaniwa ina uwezo mkubwa wa kijeshi japokuwa wanategemea misaada ya chakula kutoka nje. Umoja wa Mataifa uliiomba Korea kasakazini kutokufanya hivyo lakini ilikaidi.
Kwa sasa China iko mbali mno katika maendeleo ya makombora ya masafa marefu, ambayo yanaweza kufika popote katika nchi jiarani ya India. Kawa upande Kombora la Agni-V linaweza kushambulia miji ya Beijing na Shangai.
Hadi hivi karibuni makombora ya awali ya India yalikuwa ya masafa marefu yaliweza kusafiri umbali wa Kilometa 3500 sawa na maili 2100, lakini hili la Agni-V ni la umbali zaidi.
China haikutoa kutoa maoni yoyote juu ya uzinduzi wa kombora la India. Uzinduzi wa kombora hilo ulionyeshwa katika mkanda maalumu likiruka kutoka pwa, likiacha moshi nyuma yake nakuelekea angani.
Changamoto za Kombora Agni-V.
Likiwa angani katika hatua zake kadhaa lilionekana kuendelea na safari yake bila matatizo yoyote. Mara baada ya uzinduzi huo kituo cha habari cha india kimesema kuwa japokuwa Kombora lao limefanikiwa lakini ni vizuri kombora hilo lingerushwa likiwa katika eneo maalumu likiwa limejengewa na sio kupachikwa katika gari linalotembea.
Kawa mujibu wa maelezo kutokana na uzito wa tani 50 ni vizuri lingekuawa katika eneo maalumu lililojengwa kwa kombora hilo. Agni-V linauwezo wakubeba kichwa cha uzito wa tani 1.5 , lina urefu wa meta17.5 sawa na futi 57na limeundwa kwa kutumia teknolojia za india, likigharimu dola milioni 486.
Maafisa wa India wanasema kombora hilo linatarajiwa kufanyiwa majaribio zaidi ya matano kati ya 2014 na 2015.
Waziri Mkuu wa India apongeza.
Akizungumza baada ya jaribio hilo Waziri Mkuu wa India Dr Manmohan Sing anasema kuwa jaribio hilo limeipa sifa kubwa India na kuonyesha ubora wa jeshi lake la ulinzi na maendeleo ya kisanyansi.
Kwa sasa, India ni miongoni mwa mataifa ulimwengiuni yenye makombora hayao. Mataifa mengine ni Ufaransa, Urusi, China, Marekani .
Mwandishi.Adeladius Makwega/APE.
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman