Kongo yaituhumu Rwanda kukwamisha mazungumzo ya amani
9 Oktoba 2024Matangazo
Kauli hiyo iliyotolewa Jumanne 08.10.2024 na Waziri wa Mambo ya Nje wa Kongo, Therese Kayikwamba Wagner katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, inafuatia madai yaliyotolewa na waziri mwenzake wa Rwanda, kwamba Kongo imekataa kusaini makubaliano yaliyofikiwa mwezi Agosti, kama sehemu ya mazungumzo ya amani yanayosimamiwa na Angola.
Kongo, Umoja wa Mataifa na nchi nyingine kadhaa zinaishutumu Rwanda kwa kuwaunga mkono waasi wa M23 kwa kuwapatia wanajeshi na silaha.
Hata hivyo, Rwanda imekanusha madai hayo. Mazungumzo hayo yanafanyika kwenye mji mkuu wa Angola, Luanda kama sehemu ya mpango wa muda mrefu wa kupunguza mvutano kati ya Kongo na Rwanda.