1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kongo yapokea chanjo zaidi za Mpox kutoka Marekani

11 Septemba 2024

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imepokea dozi 50,000 ya chanjo ya ugonjwa wa homa ya nyani kutoka Marekani. Nchi hiyo tayari imepokea chanjo nyingine 200,000 zilizotolewa na Umoja wa Ulaya.

https://p.dw.com/p/4kVBf
Chanjo ya Mpox
Chanjo ya MpoxPicha: PATRICK T. FALLON/AFP

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imepokea dozi 50,000 ya chanjo ya ugonjwa wa homa ya nyani kutoka Marekani baada ya kupokea chanjo nyingine 200,000zilizotolewa na Umoja wa Ulaya. 

Kongo ni kitovu cha mripuko wa sasa wa maambukizi ya ugonjwa huo ikiripoti zaidi ya visa zaidi ya 21,500 na zaidi ya vifo 700, kwa mujibu wa taasisi ya afya ya umma nchini humo inayosimamia janga hilo. Chanjo kutoka Marekani ziliwasili jana Jumanne kwa mujibu wa balozi wa Marekani mjini Kinshasa, Lucy Tamlyn. Kwa ujumla kufikia sasa Kongo imepokea chanjo 265,000.

 

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW