1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaKorea Kaskazini

Korea Kaskazini kurusha satelaiti yake ya kwanza ya kijasusi

30 Mei 2023

Korea Kaskazini leo hii imetangaza kuwa itazindua satelaiti yake ya kwanza ya kijasusi mwezi Juni, ikisema ina lengo kufuatilia mwenendo wa kile ilichokiita mazoezi ya kijeshi ya kizembe kati ya Marekani na Korea Kusini.

https://p.dw.com/p/4RyEa
Galileo Satellitenprogramm
Picha: AP/ESA

Kauli hiyo imetolewa siku moja tu, baada ya Korea Kaskazini kutoa taarifa nyingine kuwa itafanya majaribio ya makombora Mei 31 na Juni 11 ambayo yataweza kusababisha athari katika Bahari ya Njano, Bahari ya China Mashariki na mashariki mwa Kisiwa cha Luzon cha Ufilipino.

Kufutia kitisho hicho waziri wa ulinzi wa Japan alitoa onyo la vikosi vyake kuishambulia setilaiti au kitu kingine chochote kitakachoingia katika mipaka ya taifa la Japan.

Mvutano wa sasa unaokana ni kama majibazano ya papo kwa hapo yanayotokana na kile kinachoonekana kuwa ongezeko la majiribio ya silaha ya Korea Kaskazini na mazoezi ya pamoja ya kijeshi kati ya Marekani na Korea Kusini.