1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaKorea Kusini

Korea Kaskazini yadai vijana milioni 1.4 wajiunga na jeshi

16 Oktoba 2024

Shirika la habari la serikali nchini Korea Kaskazini KCNA, limesema leo kuwa takriban vijana milioni 1.4 wakiwemo wanafunzi na viongozi wa makundi ya vijana, wamejiunga ama kurejea jeshini wiki hii.

https://p.dw.com/p/4lqTl
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un akitoa hotuba wakati wa maadhimisho ya miaka 60 ya kunazishwa kwa chuo kikuu cha ulinzi wa taifa cha Kim Jong Un mjini Pyonyang mnamo OKtoba 8, 2024
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong UnPicha: KCNA VIA KNS/AFP

KCNA imeripoti kuwa vijana hao wamejitolea kupigana katika kile kilichoitwa '' vita vitakatifu vya kumuangamiza adui kwa silaha za mapinduzi''.

Madai ya Korea Kaskazini ya kuwa na vijana zaidi ya milioni moja waliojiandikisha katika Jeshi la Wananchi la Korea ndani ya siku mbili, yanakuja wakati ambapo mvutano unaongezeka katika rasi ya Korea .

Soma pia:Korea kaskazini iko tayari kuishambulia Korea Kusini

Mwaka jana, vyombo vya habari vya nchi hiyo vilitoa madai kama hayo ya wananchi wake kujitolea kujiunga na jeshi ili kupambana na Marekani.

Hapo jana, Korea Kaskazini ililipua sehemu ya barabara na reli zinazounganisha Korea hizo mbili katika upande wake wa mpaka na kulilazimu jeshi la Korea Kusini kufyatua risasi za kutoa onyo.