1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Korea Kaskazini yafanya majaribio ya makombora mapya

19 Septemba 2024

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un ameongoza zoezi la kufanya majaribio ya makombora mapya ya masafa mafupi na makombora mengine ya kuongozwa.

https://p.dw.com/p/4kpGI
Korea Kaskazini
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un akitazama jaribio la kile KCNA ilichokitaja kama kombora jipya la kimbinu. Septemba 19, 2024.Picha: KCNA/REUTERS

Shirika la habari la serikali KCNA limeripoti kuwa kiongozi huyo ametoa wito wa kuimarisha silaha na uwezo wa nyuklia wa nchi hiyo. Kim JongUn amesema majaribio ya silaha yanahitajika kutokana na kitisho kwa usalama wa nchi hiyo. Majaribio hayo yamehusisha makombora mapya aina ya Hwasongpho-11-Da-4.5, ikiwa ni sehemu ya mfululizo wa makombora ya masafa mafupi yanayotengenezwa nchini humo na kuaminika kusafirishwa kwenda Urusi. Maafisa wa Kyiv na wataalamu huru wamesema kuna dalili kwamba baadhi ya makombora yanayotumiwa na Urusi katika vita vyake dhidi ya Ukraine yametengenezwa Korea Kaskazini. Wiki iliyopita, Korea Kaskazini pia ilizindua kituo cha kurutubisha madini ya Urani.