1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaKorea Kusini

Korea Kaskazini yafanya mkutano wa usalama wa kitaifa

15 Oktoba 2024

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un jana aliitisha mkutano mkuu wa usalama wa kitaifa na kuelekeza kuhusu mpango wa hatua za haraka za kijeshi wakati ambapo kuna ongezeko la mvutano na Korea Kusini.

https://p.dw.com/p/4lmtT
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un akitoa hotuba wakati wa maadhimisho ya miaka 60 ya kuanzishwa kwa chuo kikuu cha ulinzi wa kitaifa cha Kim Jong Un mjini Pyongyang
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong UnPicha: KCNA VIA KNS/AFP

Mkutano huo mjini Pyongyang ulihudhuriwa na maafisa wakuu wa usalama wa nchi hiyo akiwemo mkuu wa jeshi na maafisa wengine wa kijeshi pamoja na mawaziri wa usalama wa nchi na ulinzi.

Shirika la habari la KCNA limeripoti kuwa Kim alitoa mwelekeo wa hatua za haraka za kijeshi na kuelekeza kuhusu majukumu ya kutimizwa katika operesheni ya kuzuia vita na kile alichokiita utumiaji wa haki ya kujilinda.

Soma pia: Korea kaskazini iko tayari kuishambulia Korea Kusini

Mkutano huo unakuja huku Korea Kaskazini yenye silaha za nyuklia ikiishutumu Kusini kwa kurusha droni juu ya mji wake mkuu na kupeleka wanajeshi kwenye mpaka wake, huku Korea Kusini ikisema jana Jumatatu kuwa iko "tayari kabisa" kujibu ikiwa itashambuliwa.