Korea Kaskazini yafyatua makombora mawili ya masafa mafupi
1 Julai 2024Msemaji wa jeshi la Korea kusini Lee Sung-jun amesema kombora la pili lilionekana kuruka isivyo kawaida katika hatua ya awali na kuongeza kuwa kama lingelipuka angani, athari zake na vifusi vingetua Korea Kaskazini.
Korea Kaskazini inashutumiwa kwa kukiuka hatua za udhibiti wa silaha kwa kusambaza silaha kwa Urusi kutumia katika vita vyake nchini Ukraine.
Soma pia: Wanajeshi wa Korea Kaskazini wavuka mpaka wa ulinzi mkali
Uhusiano baina ya nchi hizo mbili umefikia kiwango cha chini kabisa, huku Pyongyang ikizidisha majaribio yake ya silaha na kutuma maputo ya takataka dhidi ya jirani yake Seoul.
Pyongyang tayari ilirusha maelfu ya maputo yenye takataka katika kile ilichoita ni kulipizia kisasi hatua ya Korea Kusini ya kurusha maputo yaliyokuwa na karatasi zilizoandikwa propaganda za kuipinga serikali ya Korea Kaskazini.