Korea Kusini, Poland zalaani Kaskazini kupeleka askari Urusi
24 Oktoba 2024Viongozi hao wamesema hatua hiyo ni kitisho kwa usalama wa dunia na kwamba ni ukiukaji wa moja kwa moja wa maazimio ya baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.
Soma pia: Seoul: Huenda wanajeshi wa Korea Kaskazini wanapigana Ukraine
Rais Yeol wa Korea Kusini amesema nchi yake itachukuwa hatua. "Nimeweka wazi kwamba Jamhuri ya Korea Kusini haitoruhusu hiki kifanyike na itachukua hatua zinazostahiki pamoja na Jumuiya ya Kimataifa dhidi ya ushirikiano wa kijeshi kati ya Urusi na Korea Kaskazini.'' Amesema Yeol.
Wabunge wa Korea Kusini walisema baada ya kupata taarifa kutoka shirika la ujasusi la nchi hiyo,kwamba Korea Kaskazini imepeleka wanajeshi 3,000 Urusi. Marekani pia imesema ina ushahidi unaoonesha Korea Kaskazini imetuma idadi hiyo ya wanajeshi Urusi.