SiasaIsrael
Korti ya Uholanzi yafuta marufuku ya silaha kwa Israel
13 Desemba 2024Matangazo
Mahakama mjini The Hague imetupilia mbali madai yote na kusema hakuna sababu zozote za kuweka marufuku kamili ya usafirishaji wa vifaa vya kijeshi huko Israel.
Mashirika yasiyo ya kiserikali yamedai kuwa mamlaka za Uholanzi zilikuwa zikipuuza kuzuia kile walichokiita "mauaji ya kimbari" ya Israel huko Gaza.
Hayo yakiarifiwa, Israel imeendeleza mashambulizi yake katika Ukanda wa Mashariki ya Kati.
Mnamo Ijumaa Marekani ilisema kuna dalili zinazoleta matumaini ya kupatikana makubaliano ya kusitisha mapigano kwenye mzozo huo.