SiasaUkraine
Kuleba apigia debe uanachama wa Ukraine Umoja wa Ulaya
11 Desemba 2023Matangazo
Kuleba amesema ikiwa Umoja huo utaamuwa kutounga mkono kuanzishwa mazungumzo hayo baadae wiki hii,hatua hiyo itakuwa na athari mbaya na itawavunja moyo watu wa Ukraine.
Kuleba ameyasema hayo leo Jumatatu wakati akiwasili Brussels ambako atakutana na mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya.
Amesisitiza kwamba Kiev iko kwenye mkondo wa kutimiza vigezo vinavyohitajika kujiunga na jumuiya hiyo ikiwa ni pamoja na kupambana na rushwa na kuimarisha haki za makundi ya walio wachache.
Viongozi wa Umoja wa Ulaya wanahitajika kuamuwa kwa pamoja kuhusu Ukraine ingawa tayari waziri mkuu wa Hungary Viktor Orban mara kadhaa amesema haungi mkono kaunzishwa mazungumzo hayo.