1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kura ya maoni Uturuki, raia wataka mageuzi

Sekione Kitojo13 Septemba 2010

Katika kura ya maoni ambayo ilikuwa muhimu sana kwa taifa la Uturuki, raia nchini humo wameidhinisha mageuzi ya katiba ambayo hayajawahi kufanyika katika muda wa miongo kadha.

https://p.dw.com/p/PAnQ
Waziri mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan akipiga kura yake ya maoni kuhusu mageuzi ya katiba, Septemba 12.Picha: AP

Katika  kura  ya  maoni  hapo jana  ambayo  ilikuwa  muhimu  sana nchini  Uturuki, raia wa nchi hiyo  wameidhinisha  mageuzi makubwa  ya  kikatiba  ambayo  hayajawahi  kufanyika  katika  muda wa  miongo  kadhaa.  Waziri  mkuu  Recep  Tayyip  Erdogan amewahutubia  wafuasi  wa  chama  chake  na  kusema , huo  ni ushindi  kwa  demokrasia. Katika   vifungu  karibu  26  vilivyofanyiwa mabadiliko, raia  wa  Uturuki  sasa  watakuwa  na  haki  zaidi, katika kwa  mfano  uwezekano  wa  mtu  binafsi  kupeleka   mashtaka katika  mahakama  ya  katiba. Pamoja  na  hayo  udhibiti  wa  raia katika  jeshi  umeimarishwa,  kwani  majenerali  ambao  watafanya mapinduzi  wanaweza   kwa  mara  ya  kwanza  kufikishwa   mbele ya  sheria.

Kama  katika  tamasha  la  muziki,  waziri  mkuu  Recep  Tayyip Erdogan  alisherehekea  ushindi  huo  na  wafuasi  wa  chama chake. Kila  wakati   wafuasi  hao  walikuwa  wakikatiza  hotuba ndefu  ya  ushindi   ya  waziri  huyo  mkuu.  Erdogan  amesisitiza , kwamba   si  chama , bali  ni  demokrasia   nchini  Uturuki  ambayo imeshinda  katika  kura  hii  ya  maoni. Waziri  mkuu  amesisitiza  pia maana  ya  Septemba  12, kwamba  ni  tarehe  ya  kura  ya  maoni. Tarehe  12  Septemba , mwaka  1980,  ikiwa  ni  miaka  30  kamili , jeshi  la  Uturuki  lilifanya  mapinduzi  na  matokeo  yake  ni  kile kinachojulikana  kama  katiba  ya  mapinduzi  ya  kijeshi. Na  katiba hiyo  ilikuwa  hadi  jana  ni  sehemu  kubwa  ya   katiba  ambayo haikubadilishwa  na  hivi  sasa   kwa  kupitia  matokeo  ya   kura hiyo  ya  maoni  imefanyiwa  mageuzi.

Tarehe  hii  ya Septemba  12  hadi  sasa , kupitia  katiba  iliyotokana na  mapinduzi  ya  kijeshi  ilikuwa  imechafuliwa. Kutokana  na  kura hii  ya  maoni , ambayo  imefanyika  pia  tarehe  12  Septemba , inaanza  sasa  enzi  mpya   katika  demokrasia. Tunafungua  sasa ukurasa  mpya  na  kuusafisha  uchafu  huo.

Waturuki  wamepiga  kura  kwa  wingi  wa  kushangaza  katika kuidhinisha  katiba  hiyo. Kiasi  cha  asilimia  58  ya  wapiga  kura wamesema  ndio ,  asilimia  42  wamekataa.  Hadi  hivi  karibuni watafiti  wa   maoni   ya  wapiga  kura   walitabiri  matokeo yanayokaribiana  sana .  Kiasi  cha   asilimia  78   ya  wapigakura walishiriki  katika  kura  hiyo  ya  maoni.

Kura  nyingi  za  ndio  zimepigwa  hususan  na  wapiga  kura  kutoka upande  wa  mashariki  ya  Uturuki, katika  eneo  la  Wakurdi  nchini humo. Katika  eneo  hilo  vyama  vya  Wakurdi   na  makundi  ya kijamii  yalitoa  wito  ya  kususia  kura  hiyo  ya  maoni. Katika  mji mkuu  Ankara  matokeo  yalikuwa  asilimia  57  ya  wapiga  kura wamesema  ndio, na  katika  mji  wa Istanbul  kiasi  cha  wapiga kura   asilimia  56  wamesema  ndio.

Erdogan  katika  sherehe  za   ushindi  wa  kura  hiyo  ya  maoni katika  makao  makuu  ya  chama  chake  mjini  Istanbul  amesisitiza uzalendo. Kura  hiyo   itaingia  katika  historia  ya  Uturuki, ameeleza.

Ni  lazima  watu  wawakumbukeni,  ni  lazima  watu  watukumbuke.

Kupitia  mageuzi  hayo   kutakuwa  na  sheria  kadha  za  kiraia katika  katiba  hiyo. Miongoni  mwa  hizo  ni  haki  kubwa  zaidi  kwa watoto  na  wafanyakazi,  hususan    ulinzi   wa  data  utaimarishwa . Jeshi  la  Uturuki  linapoteza  zaidi  umuhimu  wake. Majenerali ambao  wako  hai  ambao  wamefanya  mapinduzi  katika  mwaka 1980  wanaweza  kufikishwa  mahakamani,  na  hasa  mamlaka  ya mahakama  ya  kijeshi  yatawekewa  mipaka.

Zaidi  ya  hayo  bunge  la  Uturuki  litapatiwa  mamlaka  makubwa  na jopo  la  majaji  wa  mahakama  kuu   nchini  humo. Suala  hili  lilikuwa mada  muhimu   iliyokosolewa  na    upande  wa  upinzani   kuwa inaingilia  uhuru  wa  wabunge  waliochaguliwa  na  wananchi.

Washindi  dhahiri  hata  hivyo  wa   kura  hii  ya  maoni   ni  chama tawala  cha  kihafidhina  AKP  cha  waziri  mkuu  Erdogan. Kinaingia na   kura  ya  wazi  ya   ndio ,  katika  kinyang'anyiro  cha  uchaguzi wa  bunge  mwaka  ujao.

Mwandishi : Steffen  Wurzel / ZR /  Sekione  Kitojo

Mhariri:Abdul-Rahman