Labor yashinda uchaguzi mdogo wa Uingereza
3 Mei 2024Chama cha Labour kimejinyakulia jimbo la Blackpool Kusini kwa asilimia 26.3 na mgombea wake, Chriss Webb ameuita ushindi huo kuwa ujumbe kwa Conservative:
"Watu wa Blackpool Kusini wamezungumza kwa ajili ya Uingereza. Wamemwambia Rishi Sunak na Conservatives imetosha. Wamechoshwa na miaka 14 ya Conservatives kuwa madarakani, wamepoteza imani ya Waingereza. Na Blackpool nayo imechoshwa na hii serikali iliyoshindwa na kuharibu uchumi, huduma zetu za umma na kuongeza kodi. Wamesema ni wakati wa mabadiliko - na mabadiliko yameanzia hapa Blackpool usiku wa leo."
Labour yashinda viti vya ubunge katika ngome ya Conservative Uingereza
Matokeo ya awali yalionesha Labour inaweza kushinda viti vingi vya udiwani, lakini macho yote yalikuwa kwenye kinyang'anyiro cha mameya wa mikoa na wa mji mkuu, London, ambapo matokeo yanatarajiwa kutoka baadaye leo ama kesho Jumamosi.