LAGOS: Watu 50 wafa maji
2 Machi 2007Matangazo
Watu 50 wamekufa maji katika eneo la Niger Delta nchini Nigeria wakati boti walimokuwa wakisafiria lilipozama.
Boti hilo lilipinduka jana kufuatia hali mbaya ya hewa na mvua kubwa muda mfupi baada ya kuondoka Yenagoa mji mkuu wa jimbo la Bayelsa. Inasemakana boti hilo lilikuwa limebeba mizigo kupita kiasi ilichotakiwa.
Abiria wengi waliokuwa wamekimbilia sehemu ya chini ya boti hilo wakikimbia mvua walikwama na kufa wakati lilipozama.
Vyombo vya habari nchini Nigeria vimeripoti kuwa abiria wengi waliokufa ni wanawake na watoto.
Mwezi uliopita madarhezi ya watu waliuwawa wakati boti iliyokuwa njiani kwenda Nigeria ikitokea nchi jirani ya Cameroon ilipozama kwa sababu ya kubeba mizigo kupita kiasi.