SiasaUrusi
Lavrov: Nchi za Magharibi zilizuia mazungumzo na Ukraine
23 Januari 2023Matangazo
Matamashi ya Lavrov aliyoyatoa akiwa ziarani Afrika Kusini ni sawa na yale yaliyotolewa mwaka jana na Rais wa Urusi Vladmir Putin, kuwa nchi yake ilitaka kufanya mazungumzo, lakini washirika wa Magharibi walizuia hilo kufanyika.
Marekani na mataifa mengine ya Magharibi yanasema Urusi haina nia ya kufanya mazungumzo ya kumaliza vita, ambavyo mwezi ujao vitafika mwaka mmoja.
Urusi mara kadhaa inakataa masharti ya Ukraine na nchi za Magharibi kuitaka ijiondoe nchini Ukraine kama masharti ya kufanyika mazungumzo yoyote.