1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Learning by Ear – Washirika wetu ni akina nani?

3 Juni 2011

Wajue washirika wetu!

https://p.dw.com/p/RRbw

Learning by Ear ni ni mojawapo ya alama zilizoteuliwa katika shindano la "Germany – Land of Ideas" yaani Ujerumani - Nchi ya mawazo bunifu, la mwaka 2010, na msimamizi wake Rais wa zamani wa Ujerumani Horst Köhler. Kati ya maombi 2,200 kutoka kampuni mbalimbali, taasisi za utafiti, taasisi za sanaa na utamaduni, mashirika ya kijamii na yale ya kutoa misaada, waamuzi wa shindano hilo walichagua washindi kutoka vitengo saba ambao walielezea kwa ufasaha jinsi Ujerumani ilivyo jungu la mawazo bunifu.

e-Learning Africa ni mtandao ambao umepindukia kuwa na ufuasi mkubwa na kuongeza idadi ya watumiaji wake wanaotaka kuendeleza masomo kupitia mtandaoni barani Africa, mbali na kuwaunganisha wasomi kutoka maeneo mbalimbali ya ulimwengu, hivyo kuwawezesha watumiaji kupanua vipawa, kujenga uwezo na uhusiano mwema katika sekta mbalimbali za kiuchumi na mataifa ya kigeni.

“e-Taalim” ni mtandao au blogi inayotoa habari zisizoegemea upande wowote na bila malipo kwa lugha ya Kiingereza, Kiarabu na Kifaransa, hasa kwa wakuu wa mashirika mbalimbali na wasomi barani Afrika na mataifa ya Kiarabu, kuhusu matumizi ya teknolojia ya mawasiliano, mbali na kudhihirisha kwamba ni chombo cha habari cha kutegemewa siku zote. Inalenga kutoa habari mpya kuhusu mafunzo kupitia mtandao, e-learning, na elimu kwa ujumla pamoja na taasisi zinazotoa mafunzo kupitia mtandao. Kwa lugha ya Kiarabu Taalim inamaanisha elimu na "e-Taalim" ina maana elimu kupitia vifaa vya elektroniki.

Wakati wa kinyang’anyiro cha Kombe la dunia mwaka 2010 nchini Afrika Kusini shindano la Laduma baina ya shule lilikusudiwa kushirikisha mchezo wa kandanda na malengo ya milenia ya Umoja wa mataifa kwa bara la Afrika. Shule zilizotaka kushiriki ziliweza kufanya hivyo kupitia tovuti ifuatayo: www.laduma-iq.com.

Mradi wa Global 3000 unaonyesha jinsi watu wanavyoishi na fursa za kujiendeleza, manufaa na athari za utandawazi.