1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Leverkusen kukwaana na Inter Milan michuano ya Champions

10 Desemba 2024

Michuano ya Ligi ya Mabingwa inaendelea leo huku timu tatu za Ujerumani zikishuka dimbani.

https://p.dw.com/p/4nyNs
Kocha wa Bayer Leverkusen, Xabi Alonso
Kocha wa Bayer Leverkusen, Xabi Alonso. Picha: Annegret Hilse/REUTERS

Bayer Leverkusen wanakwaruzana na moja ya timu bora za Ulaya, Inter Milan ya Italia. Mabingwa hao wa sasa wa Ujerumani watalenga kuivuruga rekodi ya Inter katika mashindano ya Ulaya msimu huu kwa kuwapa kipigo cha kwanza uwanjani BayArena. Kama Inter watashinda mechi ya leo wataimarisha jitihada zao za kufuzu moja kwa moja kwenye hatua ya mtoano.

Bayern Munich watakuwa ugenini kuchuana na Shakhtar Donetsk ya Ukraine, mechi itakayochezwa mjini Gelsenkirchen Ujerumani. Bayern watakuwa bila ya mlinda lango wao na nahodha Manuel Neuer hadi mwakani baada ya kuvunjika mbavu.

Nafasi yake itachukuliwa na Daniel Peretz. Aidha miamba hao watakosa huduma za mshambuliaji wao Harry Kane, Kingsley Coman, ALphonso Davis na Serge Gnabry. 

Nao RB Leipzig hatimaye wanataka pointi zao za kwanza kwenye Ligi ya Mabingwa watakapowakaribisha Aston Villa, wakiongezwa nguvu na ushindi wa mfululizo katika ligi ya Ujerumani. Leipzig wamepoteza mechi zao tano za kwanza katika mashindano hayo ya Ulaya mpaka sasa.