Libya imekwama katika mgogoro, aonya mjumbe wa UN
16 Julai 2021Matangazo
Akizungumza katika mkutano wa Baraza la Usalama kuhusu Libya wa ngazi ya mawaziri, Kubis ameelezea wasiwasi kuhusu madhara ya mkwamo huo kwa mchakato wa uchaguzi na kisiasa.
Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa kuna zaidi ya mamluki 20,000, wakiwemo Warusi, Wasyria, Wachad na Wasudan na wanajeshi wa kigeni, wengi wao Waturuki, wanaopigana nchini Libya.
Mjumbe huyo wa Umoja wa Mataifa pia ameashiria kuwa bajeti haiwezi kuidhinishwa wiki hii na kuwa mishahara ya wahudumu kwa upande wa upinzani haijalipwa.
Mkutano huo ulihudhuriwa na Waziri Mkuu wa Libya Abdelhamid Dbeibah, Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Ufaransa Jean-Yves Le Drian, ambaye nchi yake inashikilia urais wa Baraza la Usalama kwa mwezi Julai, wamesisitiza kuwa mafanikio yanawezakana Libya.