1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaLibya

Libya, Umoja wa Ulaya kushirikiana kukomesha uhamiaji

18 Julai 2024

Libya na mataifa mengine ya Afrika na nchi za Ulaya zimekubaliana kuanzisha miradi ya uwekezaji barani Afrika kwa lengo la kuzuia uhamiaji usio wa kawaida kutoka Afrika kwenda Ulaya, wakati wa kongamano lao la uhamiaji.

https://p.dw.com/p/4iRY2
Uhamiaji wa Libya Tunisia
Wahamiaji kutoka nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara wanaodai kuwa wametelekezwa jangwani na mamlaka ya Tunisia bila maji au makazi.Picha: MAHMUD TURKIA/AFP/Getty Images

Waziri wa Mawasiliano wa Libya Walid Ellafi amesema nchi shiriki zimekubaliana kuunda "kikundi kazi" ambacho "kitatambua miradi ya maendeleo ya kipaumbele katika nchi za Afrika ambayo ni chanzo cha uhamiaji"

Mapema Jumatano, Waziri Mkuu wa Libya, Abdelhamid Dbeibah alisema Libyaina "wajibu wa kimaadili" kwa wahamiaji wengi wa eneo la  Afrika kusini mwa Jangwa la Sahara "wanaovuka jangwa na bahari" wanye matumani ya kuingia katika ardhi ya Ulaya.

Libya ambayo ipo umbali wa takriban kilomita 300 kutoka Italia, ni sehemu muhimu ya wahamiaji kuanzia safari zao, hasa kutoka nchi za kusini mwa Jangwa la Sahara, wanaohatarisha uhai kwa lengo la kuyasaka maisha bora zaidi barani Ulaya.