1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ligi kadhaa barani Ulaya kuanza kutifua vumbi leo

11 Agosti 2023

Manchester City kushuka dimbani leo dhidi ya Burnley kwenye Ligi Kuu ya Premia huku Sevilla wakiwakaribisha Valencia katika mchezo wa ufunguzi wa La Liga.

https://p.dw.com/p/4V4qe
Mechi ya fainali ya Ligi ya Mabingwa msimu uliopita kati ya Manchester City na Inter Milan
Wachezaji wa Manchester City wakishauriana na kocha wao Pep GuardiolaPicha: MIke Egerton/PA Wire/picture alliance

Baada ya karibu miezi mitatu ya mapumziko na kurejea kwa ligi mbalimbali barani Ulaya hatimaye umewadia wakati wa wapenzi wa soka kuanza tena kufurahia kandanda kwa kuanza tena ligi mbalimbali.

Soma zaidi: Baada ya zaidi ya miaka 10 ndani ya EPL, Harry Kane yupo mbioni kukamilisha hatua za mwisho kujiunga na Bayern Munich

Ligi kuu ya Premia ya nchini Uingereza inaanza kutimua vumbi leo kwa mchezo kati ya mabingwa watetezi Manchester City ambao watawafuata Burnely, mabingwa hao watetezi wataanza kutetea taji lao kwa safari ya kwenda Turf Moor na kukutana tena na nahodha wao mashuhuri Vincent Kompany.

Pande hizo mbili zilimenyana katika Kombe la FA msimu uliopita na City waliwachapwa Burnley mabao 6-0.

Siku ya Jumamosi Arsenal watacheza dhidi ya Nottingham Forest, Sheffield United na Crystal Palace, Brentford watawakaribisha Tottenham Spurs na siku ya Jumapili Chelsea watakuwa nyumbani kucheza na Liverpool.

Soma zaidi: Bayern hatimaye wavunja benki kwa ajili ya Kane 

PSG imempa mkataba Luis Enrique kuitia makali klabu hiyo ya Ufaransa
Luis Enrique, Kocha mpya wa mabingwa wa ufaransa PSGPicha: Olivier Arandel/MAXPPP/dpa/picture alliance

Nchini Ufaransa Ligue 1 leo kutashuhudiwa mchezo mmoja pia kati ya wenyeji Nice na Lille katika uwanja wa Allianz Riveira, Mabingwa Paris Saint German watawakaribisha Lorient siku ya Jumamosi huku Marseille wakiteremka dimbani kucheza na Reims.

La Liga ya nchini uhispania leo Sevilla inashuka dimbani kucheza na Valencia huku Almeria wakiwakaribisha Rayo Vallecano, Real Madrid watakuwa na kibarua cha kuwafuata Kesho Athletic Club na Barcelona watakuwa ugenini siku ya jumapili kucheza na Getafe.

Kwa wadau wa kandanda laUjerumani watasubiri hadi tarehe 18 mwezi huu ambapo ligi ya Bundesliga itaanza kwa mchezo kati ya mabingwa watetezi Bayern Munich ambao watawafuata Werder Bremen katika mchezo wa ufunguzi wa ligi.

Timu mbalimbali zimejiimarisha kwa kufanya sajili mpya ambazo wanaamini zitawasaidia katika mashindano ya ligi mbalimbali msimu huu na bado vilabu vingine vipo katika hatua za mwisho za usajili kwa wachezaji wapya kwa ajili nya kuwatumia katika michuano wanayoshiriki.