Lindner: Sio rahisi kufanya kazi na Kamala kuliko Trump
26 Julai 2024Lindner anayetokea chama cha Waliberali, FDP ameliambia gazeti la Ujerumani la Handelsblatt katika maoni yaliyochapishwa jana kuwa, baadhi ya watu wanatumai kuwa mambo yatakuwa mepesi chini ya uongozi wa Kamala Harris tofauti na Donald Trump japo yeye ana mtazamo mwengine.
Wanasiasa wengi nchini Ujerumani walionekana kuwa na ahueni kwa hatua ya Joe Biden kujiondoa kwenye kinyang'anyiro cha urais.
Lindner hata hivyo amesisitiza kuwa hatma ya uchaguzi huo utaamuliwa na wapiga kura wa Marekani.
Soma pia: Berlin kusaka mwarobaini utekelezaji wa ukomo wa deni
Waziri huyo ametahadharisha kuwa Ujerumani haipaswi kujitenga na Marekani kwani Berlin bado ina maslahi katika makubaliano ya ushirikiano wa biashara na uwekezaji kati ya Umoja wa Ulaya na Marekani.
Amesema maslahi hayo sio tu kwa sababu ya usalama lakini pia kiuchumi hasa kutokana na ushindani wa kibiashara na China.