LONDON: Amnesty International laonya hatari ya kuzuka janga
28 Agosti 2006Shirika linalotetea haki za binadamu duniani, Amnesty International,limetoa mwito kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuchukua hatua moja kwa moja kuwalinda wakazi wa jimbo la Darfur, magharibi mwa Sudan.Shirika hilo limesema vikosi vya Sudan vinavyoimarishwa Darfur,huenda vikasababisha janga kubwa kuhusu haki za binadamu.Vile vile shirika hilo linataka majeshi ya amani ya Umoja wa Mataifa yachukue nafasi ya wanajeshi 7,000 wa Umoja wa Afrika walioamua kuondoka Darfur.Rais Omar el-Bashir wa Sudan anakataa kuruhusu vikosi vya kimataifa katika jimbo la Darfur.Kiasi ya watu 300,000 wamefariki na zaidi ya milioni 2.4 wamepoteza makazi yao tangu mapigano kuzuka mapema mwaka 2003,kati ya waasi wenye asili ya Kiafrika walio wachache na serikali ya Khartoum inayodhibitiwa na Waarabu.