1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON: Shirika la Amnesty International latoa ripoti ya mwaka

23 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CBzD

Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limesema ufisadi umeendelea kushamiri barani Afrika.

Katika ripoti yake ya mwaka iliyowasilishwa hii leo, shirika hilo limesema bara la Afrika linakabilwia na umaskini uliokithiri ambao umesababisha matatizo zaidi kuhusiana na ukiukaji wa haki za bindamu.

Kiongozi wa shirika la Amnesty International mjini London, Irene Khan, amesema nchi fisadi barani Afrika zilitoa mwanya kwa taasisi za kiserikali na washikadau wa kiuchumi kufuja mali ya umma.

Aidha Bi Kahn amesema ushirikiano wa kimataifa unahitajika kupambana na ukiukaji wa haki za binadamu.

´Ukiukaji wa haki za binadamu unaweza kukomeshwa kama kutakuwepo na ushirikiano mkubwa wa kimatiafa, kama siasa za uoga zitakwisha na kama kutakuwa na hisia ua thamini haki za binadamu. Tuamini kwamba dunia iliyogawanyika inaweza kuunganishwa pamoja na maadili ya kimataifa ya haki za biandamu.´

Kwa mujibu wa ripoti ya shirika la Amnesty International, China, Vietnam, Saudi Arabia, Irak na Uturuki zimezokosolewa kwa ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu na kubana uhuru wa kuabudu.