LONDON:Waislamu waunga mkono mpango wa kuwarejesha makwao wahubiri siasa ya chuki ya dini
18 Septemba 2005Waislamu wengi nchini Uingereza wanaunga mkono mpango wa serikali wa kuwarejesha kwenye nchi zao watu wanaohubiri siasa kali za kidini nchini humo.
Kwa mujibu wa uchunguzi uliochapishwa leo nchini humo waingereza wengi waliowaislamu wanasema kwamba wahubiri hao huenda wakawatia moyo washambuliaji wa kujitoa muhanga kama wale waliofanya mashambulio dhidi ya vituo vya magari ya moshi ya chini ya ardhi mjini London mnamo mwezi wa July.
Uingereza imesema kwamba Watu kumi waliokamatwa mwezi uliopita nchini humo akiwemo kiongozi wa kidini anayeshukiwa kuhusiana na Alqaeda barani Ulaya Abu Qatada mzaliwa wa Jordan,watarejeshwa katika nchi zao.
Wanaharakati wakutetea haki za raia wanasema wanatilia shaka mpango huo wa serikali wakisema kuwa huenda watu hao wakakabiliwa na mateso kwenye nchi watakazorejeshwa.