Lufthansa yasitisha safari za ndege Tehran
11 Aprili 2024Matangazo
Eneo hilo lipo katika tahadhari ya uwezekano wa Iran kufanya mashambulizi ya kulipiza kisasi kutokana na shambulio la anga la Israel dhidi ya ubalozi wa Tehran nchini Syria.
Taarifa ya shirika hilo imesema kuwa wanasimamisha safari za ndege za kwenda na kutoka Tehran kutoka Aprili 6 hadi pengine Aprili 11.
Biden: Sikubaliani na mbinu za Netanyahu huko Gaza
Baadhi ya nchi katika kanda hiyo, ikiwemo Marekani zimekuwa katika hali ya tahadhari na kujiandaa kwa mashambulizi yanayoweza kufanywa na Iran tangu Aprili mosi.
Kiongozi mkuu wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei, alisema kuwa Israel lazima iadhibiwe kwa shambulio la Damascus ambalo liliwaua maafisa saba wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi.