1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Lungu: Tusifuate mfano wa Kenya

3 Novemba 2017

Rais Edgar Lungu wa Zambia amewaonya majaji nchini humo dhidi ya uamuzi wowote watakaotoa kumzuia asiwanie tena nafasi ya urais katika uchaguzi utakaofanyika mwaka 2021. Wapinzani wasema anakiuka katiba.

https://p.dw.com/p/2mxfE
Edgar Lungu rais wa Zambia
Picha: picture-alliance/P.Wojazer

Amesema hatua kama hiyo ya mahakama ilitaka kuingiza Kenya katika machafuko ya kisiasa. Rais Lungu anatarajiwa kuwania nafasi hiyo katika uchaguzi wa mwaka 2021, lakini anaweza akakabiliwa na pingamizi la kisheria kutoka vyama vya upinzani vinavyodai kuwa itakuwa ni kinyume cha katiba, kwa vile kiongozi huyo atakuwa tayari ametumikia vipindi viwili vya uongozi, ambavyo vinaruhusiwa kisheria.

Lungu ameyasema hayo wakati alipokuwa akiwahutubia wafuasi wake katika mji wa Solwezi kaskazini magharibi mwa nchi hiyo katika hotuba iliyotangazwa moja kwa moja  na redio ya taifa, akisema hata hivyo hakusudii kuitisha idara ya mahakama. Onyo hilo la Lungu linakuja baada ya Kenya kukumbwa na mgogoro mkubwa wa kisiasa katika kipindi cha miezi miwili kufuatia Mahakama ya Juu nchini humo kuyafuta matokeo ya uchaguzi wa rais wa mwezi Agosti kutokana na kubainika kukumbwa na kasoro kadhaa.