Maafisa wa Kenya waenda Dubai kufuatilia kashfa ya dhahabu
21 Mei 2019Matangazo
Wakati huohuo, pirikapirika zinaripotiwa bungeni za kusaka saini ili kumtimua waziri wa usalama wa taifa, Fred Matiangi, kwa madai ya kuwalinda watuhumiwa wa kashfa hiyo.
Polisi nao wanashikilia kuwa maafisa wao waliokuwako kwenye eneo ilikopatikana dhahabu hiyo bandia walikuwa wanawalinda wanadiplomasia na wala sio wahalifu.
Maafisa wa idara ya ujasusi walitazamiwa kusafiri jioni ya Jumanne (21 Mei) kuelekea Dubai ili kuchukuwa taarifa ya mwakilishi wa Umoja wa Falme za Kiarabu kuhusu sakata hilo la dhahabu bandia linalochunguzwa.
Majasusi hao walitazamiwa kumhoji Ali Zandi anayemuwakilisha Sheikh Mohammed bin Rashid Al Maktoum na kampuni ya Zlivia inayofanya biashara ya dhahabu Dubai.