1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaUfaransa

Idadi ya vifo vilivyotokana na kimbunga Chido yafika watu 39

25 Desemba 2024

Maafisa wa Ufaransa wameongeza idadi ya vifo vilivyotokana na kimbunga Chido katika visiwa vya Mayotte kutoka 35 hadi 39, siku kumi baada ya visiwa hivyo kukumbwa na kimbunga hicho.

https://p.dw.com/p/4oYtr
Mayotte | Chido
Uharibifu uliofanya na kimbunga Chido visiwani MayottePicha: Adrienne Surprenant/AP/dpa/picture alliance

Mamlaka hata hivyo imesema maelfu ya watu huenda wamepoteza maisha kufuatia kimbunga hicho.

Mamlaka imeongeza kuwa shughuli ya kuhesabu watu waliofariki inaweza kukumbwa na changamoto kutokana na baadhi ya watu kuwazika wapendwa haraka kulingana na mafundisho ya kidini, na pia kwa sababu wengi waliofariki walikuwa wahamiaji wasiokuwa na vibali.

Soma pia:  Ufaransa yafanya maombolezo ya wahanga wa kimbunga huko Mayotte

Kasi ndogo ya kupeleka misaada visiwani humo imewakasirisha wenyeji wa Mayotte, eneo maskini zaidi lililoko chini ya Ufaransa.

Ama kwa upande wa Msumbiji, nchi hiyo imeripoti vifo vya watu 94 vilivyotokana na kimbunga hicho wakati nchi Jirani ya Malawi ikiripoti vifo 13.