Maafisa wanne wa polisi wauawa Port-au-Prince
1 Machi 2024Kiongozi mashuhuri wa genge alisema mashambulizi yaliyoratibiwa na makundi yenye silaha yangeliendelea kwa lengo la kumtimua madarakani Waziri Mkuu Ariel Henry.
Milio ya risasi ilisikika katika jiji lote huku vikosi vya usalama vikipambana na washambuliaji waliokuwa wamelenga vituo vya polisi, vikiwemo viwili vilivyochomwa moto.
Maeneo mengine yaliyoshambuliwa namagenge hayo ni chuo cha polisi na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Toussaint-Louverture.
Soma zaidi: Mahakama Kenya yaizuwia serikali kupeleka askari Haiti
Afisa wa chama cha polisi aliliambia shirika la habari la AFP kuwa pamoja na maafisa wanne waliouawa, watano wengine walijeruhiwa.
Hayo yalijiri wakati Waziri Mkuu Henry akiwa nchini Kenya ambako nchi hizo mbili zilisaini makubaliano ya kujaribu kuokoa mpango wa taifa hilo la Afrika kupeleka polisi wake 1,000 nchini Haiti.
Kikosi hicho cha polisi ya kimataifa kilikusuiwa kuisaidia Haiti kupambana na magenge hayo yanayofanya uhalifu kwa viwango visivyo na kifani.