1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maandamano dhidi ya Netanyahu yafanyika Israel

12 Aprili 2024

Waandamanaji walimiminika mitaani kwenye viunga vya mji mkuu wa Israel, Tel Aviv, kupaza sauti za kuikosoa serikali ya waziri mkuu Benjamin Netanyahu na kutoa wito wa kuachiwa huru mateka wanaoshikiliwa na Hamas, Gaza.

https://p.dw.com/p/4egvl
Benjamin Netanyahu
Maandamano dhidi ya Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu yafanyika Tel Aviv Picha: Amir Levy/Getty Images

Wengi walikuwa wamebeba mabango makubwa yenye picha za mateka ambao inaaminika bado wanashikiliwa na Hamas ndani ya Ukanda wa Gaza tangu walipokamatwa wakati wa shambulio dhidi ya Israel, Oktoba 7 mwaka jana. 

Maandamano hayo yanafuatia mengine makubwa yaliyofanyika mwanzoni mwa mwezi huu mjini Jerusalem katika kile kinachoonekana kuwa migawanyiko miongoni mwa Waisraeli hasa kuhusu namna waziri mkuu Netanyahu anavyoushughulikia mzozo wa nchi hiyo na kundi la Hamas.

Maandamano dhidi ya serikali yatanda Israel

Tayari shinikizo linaongezeka la kutaka kuitishwe uchaguzi wa mapema ambao Netanyahu amesema utavuruga kampeni yake ya dhidi ya Hamas na kukwamisha mazungumzo ya kuachiwa kwa mateka.