Machafuko Burundi
Tangu Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza atangaze nia yake ya kuwania tena urais, taifa hilo limekabiliwa na vurugu kati ya waandamanaji na polisi. Mpiga picha wa AFP Phil Moore ameshuhudia vurugu hizo.
Mgogoro unaonekana
Tangu mwanzo, mambo yalikuwa wazi kuwa uchaguzi wa Burudi utakuwa na ubishani, kwa upingwaji mkubwa wa rais Nkurunziza kuwania muhula wa tatu. Katika wakati ambapo chama chake cha CNDD-FDD, kinanafanya uteuzi, Nilikuwa katika jukumu la kikazi katika taifa jirani la DRC lakini nikifuatilia hali ilivyokuwa. Kwa hivyo nilipaswa kusafiri haraka iwezekanavyo kwenda Bujumbura Alhamisi ya Mei 1,2015.
Kifo cha kwanza
Siku niliyofika, vyama vya kiraia vilisimamisha maandamano, ilikuwa mwishoni mwa juma, nikajaribu kufanya udadisi wa kinachoendelea nchini humo. Siku ya kwanza kulifanyika mazishi ya Jean-Claude Niyonzima, ambae aliuwawa siku ya kwanza ya maandamano, Aprili 26,2015. Familia yake ilisema watu wenye silaha waliingia katika nyumba yake na kumfyatulia risasi.
Kupigwa risasi mgongoni
Siku mbili baadae nilikuwa katika kituo kitogo cha afya katika kitongoji cha Musaga- kitovu cha maandamano ambapo kijana niliyemtambua kama Pascal alipoteza damu nyingi. Alifikwa na mkasa kama unaoonekana tukio la kupigwa risasi mgongon katika maandamano. Pascal alikuwa hajitambui. Baadae nikapata taarifa ya kifo chake. Msemaji wa wizara alidai kuwa polisi haikutumia silaha za moto.
Hatari kazini
Nilikuwa nafanya kazi katika mazingira ambayo maafisa usalama walikuwa wakali sana kwa vyombo vya habari, na makundi yanaweza kufanya vurugu wakati wowote. Lakini kwa kiasi kikubwa hilo halikufanyika katika mji mkuu wa Burundi, ingawa wengi wa 'Imbonerakure,' tawi la vijana la chama tawala ambalo linapinga maandamano, wamekaidi kuzungumza na wamekuwa wakichukizwa na hatua ya kupigwa picha.
Pande mbili za vizuizi
Nimetumia muda mwingi wa kuzungumza na kuwa na muingiliano na polisi na waandamanaji. Kupiga picha zenye kuelezea hali halisi, naamini lazima uelewe mwenendeo wa matukio yalivyo. Kwa mara kadhaa polisi walinuliza mimi: “Unaonaje hali ilivyo hapa?” na ukivuka vizuizi, waandamanaji wanakuuliza swali kama hilo.
Hasira na kuchoshwa
Waandamanaji wamegadhibishwa na kitencho va Nkurunziza, kukiuka katiba kuwania tena urais. Kumekuwa na kuchanganyikiwa kwa kiasi kikubwa sana na hali hiyo, ilichochewa zaidi na vurugu za polisi. Idadi kubwa ya maduka imefungwa. Vilevile, kitendo cha kununua chakula kumezidi kuwa kigumu sana. Na kwa sababu ya kutokuwa na uhakika wa hali ya usalama wengi wanatumia nyakati usiku katika ulinzi.
Ndege aliyechukiwa
Chama tawala CNDD-FDD, ambacho kimemteuwa Nkurunziza kuwa mgombea wake kina picha ya tai kama nembo yake. Waandamanaji wamebeba mabango yenye picha ya taswira hiyo juu ya msalaba mwekendu kukikebehi. Kitendo cha kushtusha zaidi kwa waandamanaji kilikuwa cha kunyonyoa kile kilichoonekana kama jogoo aliekufa. Walimshika kuku huyo mbele kabisa ya maandamano wakiwapungia polisi waliokuwa mbele yao.
Igizo la upinzani
Kama ilivyo namna ya kujipamba, waandamanaji wengi zaidi katika maeneo ya vizuizi walionekana kujipaka masizi usoni. Wengine walianza kuvaa vinyago, kujifunika kwa vitambaa au kujifunika na matawi ya miti. Ilikuwa swali kubwa sana kichwani kwangu kwa mtindo wa kuficha utambulisho wao. Vipengele vya uigizaji vinachukua nafasi muhimu katika uanaharakati.
Bundiki bandia dhidi risasi za moto
Nilikuwa natembea karibu naeneo karibu na mitaa iliyohamwa na watu ya Musaga ambapo nilimuona mtu huyu alikuwa akininyemelea mimi akiwa na bunduki aina ya rifle iliyotengenezwa kwa mbao. Nilichukua kamera yangu. Bwana huyo alinitambua na kubadilisha mkao. Waandamanaji wanaonekana wenye kutumia vitisho vya bunduki bandia kujikinga na mauwaji.