Machafuko mabaya yaikumba Haiti
6 Machi 2024Ghasia hizo zinatokea wakati taifa hilo likitengwa zaidi kimataifa kufuatia shambulio kwenye uwanja wa ndege na kutoroka kwa wafungwa jela.
Lionel Lazarre, afisa kutoka chama cha polisi cha Haiti, amesema shambulio dhidi ya taasisi hiyo, ambapo zaidi ya makuruta 800 wa polisi wanapata mafunzo, lilitibuliwa baada ya kuwasili kwa maafisa wa usalama wa ziada.
Soma pia: Kiongozi wa Haiti atua Puerto Rico akijaribu kurudi nyumbani
Ghasia za hivi karibuni nchini humo, zimefuatia kuhamishwa kwa maelfu ya wakaazi kutoka mji huo mkuu huku Umoja wa Mataifa na Marekani zikielezea wasiwasi wao juu ya mzozo huo na magenge yenye silaha yakitangaza shambulio lililoratibiwa la kumtimua waziri mkuu wa nchi hiyo Ariel Henry.
Magenge hayo yanasema yanataka kuipindua serikali ya Henry, aliyekuwa nchini Kenya wikendi iliyopita kushinikza kupelekwa haraka kwa ujumbe wa polisi wa kimataifa unaoungwa mkono na Umoja wa Mataifa kusaidia kuleta utulivu nchini mwake.