Macron aagiza usalama kuimarishwa Ufaransa
14 Oktoba 2023Tukio hilo linalohusishwa na itikadi kali za kiislamu lilitokea baada ya kijana wa miaka 20 kumchoma kisu mwalimu huyo na kuwajeruhi vibaya watu wengine wawili kwenye mji wa Arras. Kufikia sasa watu kumi wamekamtwa.
Soma pia: Polisi Ufaransa wafanya misako baada ya mwalimu kuchinjwa
Kulingana na ofisi ya Macron, wanajeshi hao wa kuimarisha usalama watasambazwa kuanzia Jumatatu, kama sehemu ya operesheni inayoendelea ambayo hulinda doria katikati mwa miji mikubwa na maeneo ya utalii.
Tahadhari za kiusalama zinaendelea pia kuchukuliwa wakati nchi hiyo ikiwa ni mwenyeji wa kombe la dunia wa mchezo wa Raga.
Ufaransa imekuwa ikilengwa na mfululizo wa mashambulizi yanayohusishwa na itikadi kali za kiislamu kwa miaka mingi. Moja ya matukio mabaya zaidi lilikuwa Novemba 2015 ambapo watu wenye silaha na washambuliaji wa kujitoa muhanga kwa wakati mmoja walishambulia kumbi za starehe na migawaha mjini Paris.