1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUfaransa

Macron ahimiza kuondolewa kwa vizuizi dhidi ya Caledonia

18 Juni 2024

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ataka kuondolewa kwa vikwazo huko New Caledonia.

https://p.dw.com/p/4hBKP
Emmanuel Macron, rais wa Ufaransa
Emmanuel Macron, rais wa UfaransaPicha: Stephane De Sakutin/AFP/Getty Images

Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron amewaomba wakazi wa Caledonia kuondoa vizuizi baada ya wiki kadhaa za ghasia na kusema hali kama hiyo bado haikubaliki.

Macron kwenye matamshi yake mbele ya hadhara, alitoa wito wa kuondolewa kwa vizuizi hivyo na kulaani machafuko yaliyoshuhudiwa.

Katika barua yake iliyochapishwa na gazeti moja la New Caledonia, Macron aidha alitoa wito wa mazungumzo na kujizuia.

New Caledonia inayopakana na Australia na Fiji imekuwa chini ya utawala wa Ufaransa tangu karne ya 19, lakini jamii ya asili ya Wakanaki inataka uhuru zaidi.