1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Macron atangaza kulivunja bunge la taifa la Ufaransa

10 Juni 2024

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amesema ameamua kulivunja Bunge na kuitisha uchaguzi baada ya chama chake kushindwa vibaya katika uchaguzi wa Bunge la Ulaya.

https://p.dw.com/p/4gqp1
Frankreich TV-Ansprache Emmanuel Macron über Neuwahlen
Picha hii inamuonyesha Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron akizungumza wakati wa hotuba yake kwa taifa kwenye televisheni ambapo alitangaza kulivunja Bunge la Ufaransa na kuitisha uchaguzi mkuu mpya Juni 30.Picha: Ludovic MARIN/AFP

Akilihutubia taifa kutoka katika makazi ya rais ya Élysée jijini Paris, Macron amesema ameamua kurejesha chaguo la hatma ya bunge kupitia kura.

Kwa hivyo analivunja Bunge la Taifa, uchaguzi utafanyika kwa awamu mbili Juni 30 na Julai 7.

Hatua hiyo ni baada ya duru kutoka Ufaransa kuonesha chama cha mrengo wa kulia cha National Rally kiko mbele zaidi katika uchaguzi wa bunge wa Umoja wa Ulaya kuwashinda washirika wa Macron wanaounga mkono Ulaya.