Macron ziarani nchini Sweden
30 Januari 2024Matangazo
Mapema leo mchana, Macron akiwa pamoja na mkewe Brigitte walilakiwa na mfalme Carl XVI kwa heshima ya gwaride la kijeshi katika hafla iliyofanyika kwenye kasri la nchi hiyo mjini Stockholm.
Akizungumza na mfalme Carl Gustaf, Macron amesema ananuwia kuimarisha uhusiano kati ya Ufaransa na Sweden, mshikamano ndani ya Umoja wa Ulaya hasa wakati Sweden inakaribia kuingia ndani ya Jumuiya ya NATO.
Soma pia:Urusi na Ukraine zashambuliana usiku wa kuamkia leo
Anatarajiwa jioni hii kuwa na mazingumzo na waziri mkuu Ulf Kristersson na baadae watajiunga na Mfalme Gustaf kujadili hatma ya usalama barani Ulaya kwenye chuo cha kijeshi mjini Stockholm.