MADA KUU ZA WAHARIRI LEO NI MKUTANO KATI YA CHAMA-TAWALA SPD NA VYAMA VYA WAFANYIKAZI-ISHARA ZA KUSTAWI UCHUMI WA UJERUMANI NA ZIARA IJAYO YA SCHRÖDER MOSCOW
7 Julai 2004GAZETINI 07-07-04
Ama kuhusu mvutano kati ya chama-tawala cha SPD na vyama vya wafanyikazi gazeti la FRANKFURTER RUNDSCHAU laandika:
"Tayari hii leo kanuni ya zamani imegeuka kinyume chake kwa pande zote mbili:Tusishikamane tena bali tukitengana itaturahisishia kazi tangu kwa chama cha SPD hata kwa Shirikisho la vyama vya wafanyikazi .
Mkuu wa chama cha wafanyikazi cha VERDI Frank Bsirske humshambulia Kanzela Schröder na watu hushangiria.Na Schröder nae hawezi asipendeze mno akimhujumu hasimu wa vyombo vya habari kwa ridhaa ya kimya-kimya ya wananchi.Yamkinika vyama vya wafanyikazi kwa kubadili msimamo wao kidogo vimetaka kuepusha kuporomoka kabisa kwa serikali ya sasa ya Muungano wa vyama vya SPD na walinzi-mazingira chama cha KIJANI."
DIE WELT linamurika hasa hali anayojikuta Kanzela Schröder katika patashika hii:
Schröder,lasema gazeti- amejiweka katika hadhi leo ambayo aonekana ameiacha bendera ya kuwatetea wanyonge na ametoa sasa sura kuwa kanzela mvuta sigaa.Wivu wa viongozi wenzake chamani kwa Kanzela huyo ni ishara dhahiri-shahiri kwamba anawaachamkono.Swali ,lauliza gazeti:Je,Schröder sasa ameshindwa kuongoza.La, hasha,wasema wengine, wanaomkosoa wamekosea.kwani, Schröder hataki kuyumbishwa na ametia nia kufuata mkondo wa siasa zake pale pale.Pengine kule alikoazimia kwenda ameshawasili.Kwani chama cha SPD hakioneshi kiko tayari kwenda umbali zaidi."
Hilo lilikua DIE WELT:
BERLINER MORGENPOST laandika kuwa, muda mrefu ilitupasa kusubiri kufufuka kwa uchumi tulikoahidiwa na sasa wakati kweli umewadia.katika hali ya kustawi pole pole kwa uchumi wa dunia,uchumi pia wa Ujerumani, maarufu duniani kwa kusafirisha bidhaa zake nje unaanza kustawi.hali i8kitengemaa kwa wengine, inatengemaa pia kwetu-laandika gazeti.
Taasisi moja hadi nyengine ya kiuchumi zimekuwa zikirekebisha ukuaji wa uchumi wa Ujerumani tena kwendea juu.Na hii inaweka wazi: kustawi huku sasa kwa uchumi wa Ujerumani kunakokotwa na bidhaa zake inazosafirisha n’gambo.Biashara ya wanunuzi ndani ya nchi bado inazorota.Jinsi imani ya wanunuzi ilivyoanguka kutokana na miaka kadhaa ya msukosuko ,hofu za kujikuta hawana kazi wala bazi ni kubwa mno."
Ama gazeti la BERLINER ZEITUNG laandika:
"jibu wazi taasisi hizo za wataalamu wa kiuchumi hazitoi:imani ya wanunuzi itokee wapi wakati matarajio ya kupatikana nafasi za kazi si mazuri ?
Si ajabu Ujerumani imetumbukia katika shimo la uchumi na taabu kutoka.Baadhi wanadai-hapa paka anautafuna mkia wake.Kuanzisha wiki ya kufanya kazi kwa masaa 50 kama vile baadhi wanavyodai,hakutatatua pia tatizo hili."
Kwa jicho la mkutano ujao kati ya Kanzela Gerhard Schröder na rais Wladmir Putin mjini Moscow, gazeti la biashara kutzoka Düsseldorf-HANDELSBLATT laandika:
"Kila uhusiano wa kisiasa ukiwa mkubwa, ndipo maingiliano ya kiuchumi yanapozidi na ndipo Russia inapofungamana zaidi na UU na kujumuishwa na Shirika la Biashara duniani (WTO ).Kwa njia hii ndio matumaini ya utulivu wa kisiasa yanapoongezeka.
Na hii inapunguza hatari ya uwezekano wa siku moja kufunga bomba lake la gesi isije Ujerumani. Hatahivyo, mazungumzo kati ya Berlin na Moscow,yanahitaji kukosoana. Wazi wakati wa ziara yake hii,Kanzela Schröder anapaswa kuzindua kwamba ushirika wa kimbinu unahitaji kuwapo imani na dola kuheshimu sheria.Schröder pia anapaswa kukumbusha kwamba mfumo imara,huru na wa kidemokrasia ndio unaotoa mwanya wa biashara ya soko huru kustawi na kunawiri...."