1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Madaktari wanataka Michezo ya Rio ifutwe

28 Mei 2016

Zaidi ya wataalamu 100 wa afya, wanazuoni na wanasayansi Ijumaa (27.05.2016) wametoa wito kuahirishwa michezo ya olimpiki mjini Rio kwa kuwa tukio hilo linaweza kuharakisha kusambaa kwa virusi vya Zika duniani.

https://p.dw.com/p/1IwES
Brasilien, Olympische Spiele 2016 Symbolbild
Picha: picture-alliance/dpa/M. Kappeler

Tathmini yao inapingana na mawazo ya baadhi ya wataalamu waandamizi wa magonjwa ya kuambukiza ambao wanasema iwapo patachukuliwa hatua za tahadhari hakuna sababu ya kufuta michezo hiyo. Siku ya Alhamis, Dr. Tom Friedeb, mkurugenzi wa kituo cha Marekani kwa ajili ya udhibiti wa magonjwa na kuzuwia, alitangaza kwamba hakuna sababu ya kiafya kwa jamii hata kufuta ama kuchelewesha michezo hiyo inayotarajiwa kufanyika majira ya kiangazi.

Brasilien Margaret Chan in Recife
Mkurugenzi wa shirika la afya ulimwenguni WHO Margaret ChanPicha: Reuters/U. Marcelino

Katika barua ya wazi iliyowekwa katika mtandao wa internet, kundi hilo la wa wataalamu wa afya 150 , wengi wao wakihusika na masuala ya bakteria amesema kitisho cha maambukizi kutokana na virusi vya Zika ni cha juu kabisa. Barua hiyo ilitumwa mwa Dr. Margaret Chan, mkurugenzi mkuu wa shirika la afya ulimwenguni WHO, na kushauri kuwa michezo hiyo, ambayo inatarajiwa kufanyika mjini Rio de Janeiro mwezi Agosti , ihamishiwe sehemu nyingine ama icheleweshwe.

"Hatari bila sababu ipo wakati watalii wa kigeni 500,000 kutoka nchi zote zinazohudhuria michezo hiyo,wakipata virusi hivyo, na kurejea nyumbani kwao ambako mgonjwa huo unaweza kuwa maafa," barua hiyo imesema.

Zika Virus
Wataalamu wakifanya utafiti kuhusu virusi vya ZikaPicha: Reuters/I. Alvarado

Hatari ni kubwa

Wataalamu hao wa tabia za uhai ,Bioethicists, wanajifunza kuhusu matatizo ya kimaadili kutoka katika utafiti wa kibiolojia ama kiganga. Profesa Arthur Caplan, mkurugenzi wa kitengo cha maadili ya utabibu katika chuo kikuu cha mjini New York cha udaktari na mmoja kati ya wataalamu wanne ambao wameandika barua hiyo, amesema ana shaka iwapo Brazil ina vifaa vya kuweza kuulinda umma na wakati huo huo ana shaka ya "uhakika wa jumla " kutoka maafisa wa afya ya umma.

Brasilien - Forschung Zika Virus - Elektronenmikroskop
Uchunguzi kuhusu virusi vya ZikaPicha: Reuters/Centers for Disease Control

Barua hiyo imetoa wito kwa shirika la afya WHO kuunda kundi huru litakalotoa ushauri kwa shirika hilo na kamati ya kimataifa ya olimpiki. "Naamini kuhusu kuridhia baada ya kupata habari," Caplan amesema katika mahojiano. "Tuwe na kikundi cha wanasayansi huru watakaoangalia kuhusu hili na kumpa kila mtu nafasi ya kusikia mawazo tofauti."

Ikidokeza kuhusu "wasiwasi mkubwa kwa ajili ya afya duniani", barua hiyo pia imesema , "Virusi vya Brazil vya Zika vinaathiri afya kwa njia ambayo sayansi haijachunguza hapo kabla." Akizungumza katika chakula cha mchana katika klabu ya taifa ya waandishi habari mjini Washington siku ya Alhamis, Frieden amesema hakuna sababu ya kuchelewesha michezo ya Olimpiki.

Gelbfiebermücken
Mbu wanaoambukiza virusi vya ZikaPicha: picture alliance/dpa/A. Weigel

Alikuwa akitoa maelezo kuhusu kujibu waraka wa profesa mmoja wa Canada uliochapishwa mapema mwezi huu katika mapitio ya afya ya jarida la Harvard ambao umetoa wito wa michezo hiyo kufutwa ama ihamishiwe kwingine kwasababu inaweza kuwa chombo cha kusambaza virusi vya Zika.

"Hatari sio lazima kuwa iko juu kuliko kwa mwanamke mjamzito," Frieden amesema. Maambukizi ya Zika kwa mwanamke mjamzito yameonesha kuwa ni sababu ya kuzaliwa watoto wenye athari pamoja na watoto wenye matatizo makubwa ya ubongo.

Mwandishi: Sekione Kitojo / rtre

Mhariri: Bruce Amani