1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Zaidi ya malori 3,000 yakwama mpakani wa Poland na Ukraine

19 Novemba 2023

Zaidi ya malori 3,000 mengi yakiwa ni ya Ukraine yamekwama kwenye upande wa mpaka wa Poland hadi mapema hii leo, baada ya madereva wa malori wa Poland kufunga njia kwa siku kumi.

https://p.dw.com/p/4Z9Ag
Msururu mrefu wa malori katika mpaka kati ya Poland na Ukraine
Malori yakisubiri kuvuka mpaka wa Ukraine na Poland, huku mashambulizi ya Urusi dhidi ya Ukraine yakiendelea, katika kituo cha ukaguzi cha Rava-Ruska, eneo la Lviv, Ukraine, Aprili 17, 2023.Picha: Roman Baluk/REUTERS

Naibu Waziri Mkuu wa Ukraine Oleksandr Kubrakov ameandika kupitia ukurasa wa X kwamba, kizuizi hicho kimewafanya maelfu ya watu kuishi maisha magumu, kutokana na upungufu wa chakula, maji na mafuta. 

Maafisa wa Ukraine walisema wiki iliyopita kwamba Kyiv na Warsaw kwa mara nyingine walishindwa kukubaliana juu ya kuukabili mzozo huo.

Madereva hao wa malori wa Poland mapema mwezi huu walifunga barabara kwenye vivuko vitatu vya mpaka wa Poland na Ukraine, wakipinga kile wanachoona ni kama serikali kutochukua hatua za kuwadhibiti wafanyabiashara wageni wanaochukua biashara zao, tangu Urusi ilipoivamia Ukraine, Februari 2022.